Richard Reynolds

Richard Reynolds (Devon, 1492 hivi - Tyburn, 4 Mei 1535) alikuwa padri mmonaki wa shirika la Mt. Brigida nchini Uingereza[1].

Kwa kukiri imani ya mababu na kwa kukataa kiapo cha kumtii mfalme Henri VIII kama mkuu wa Kanisa Uingereza badala ya Papa alinyongwa ila kabla hajafa alikatwa vipandevipande ambayo vilitundikwa sehemu mbalimbali za mji. Pamoja naye waliuawa mapriori watatu wa Wakartusi, Yohane Houghton, Robati Lawrence na Augustino Webster, mbali ya paroko mwanajimbo Yohane Haile.

Alitangazwa mwenye heri na Papa Leo XIII tarehe 9 Desemba 1886 na mtakatifu tarehe 25 Oktoba 1970 na Papa Paulo VI[2].

Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe ya kifodini chake[3].

  1. "About St. Richard Reynolds", St. Richard Reynolds Catholic College Archived 16 Machi 2013 at the Wayback Machine
  2. "Biography: Forty Martyrs (RC) of England and Wales (25 Oct 1570)". elvis.rowan.edu. Iliwekwa mnamo 2020-05-04.
  3. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne